Mwanaanga wa kwanza wa Marekani kuizunguka dunia afariki




Mwanaanga wa kwanza wa Marekani kuizunguka dunia kupitia mzingo wake, John Glenn amefariki dunia akiwa na miaka 95.



John Glenn akijiandaa kusafiri kwenda angani enzi za uhai wake

Mzee huyo ambaye pia aliwahi kuwa Seneta wa mji wa Ohio kwa miaka 24 kupitia chama cha Democratic amefariki Alhamisi hii katika hospitali ya Ohio State University Wexner Medical Center, Columbus alipokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja huku chanzo cha ugonjwa wake hakijatajwa.

Glenn aliwahi kutunukiwa tuzo ya dhahabu (Congressional Gold Medal) na Rais Barack Obama, mwaka 2011. Lakini pia mwaka 1998 aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mwenye umri mkubwa kwenda angani akiwa na miaka 77.

John anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Arlington, Virginia.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment