Muimbaji mkongwe wa muziki, Mwasiti Almas amefunguka na kuuzungumzia ujio wake mpya baada ya kupata management mpya ambayo itakuwa inamsimamia yeye pamoja na kazi zake.
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Mwasiti amesema katika hatua ya awali ameanza kulififanya jina lake kuwa brand pamoja na kutambulisha logo yake mpya.
“Nataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye sehemu nyingi nyingi za jina langu kuwa brand rasmi pamoja na career yangu pia kwa ujumla,” alisema Mwasiti. “Kwahiyo kuna makubwa yanakuja kwasababu nipo na management mpya ambayo inasimamia kazi zangu kwa sasa na ipo tayari kwajili ya kumbrand upya Mwasiti,”
Aliongeza,”Kwahiyo kuna mengi yanakuja ukiachana na kuonyesha logo ya brand yangu, pia katika kazi zangu na mambo mengine. Kwahiyo ningependa kuwaambia mashabiki wangu wakae mkao wa kula katika mitandao yangu ya kijamii kutakuwa na mambo mengi na taarifa mbalimbali kuhusu ujio wangu,”
Muimbaji huyo ambaye ni zao la THT, kwa sasa bado anafanya vizuri na wimbo ‘Sema Nae’ ambao aliuachia miezi kadhaa iliyopita.
CREDIT BONGO 5
0 comments:
Post a Comment