Ronaldo ajitengenezea rekodi yake mpya kwenye soka


Cristiano Ronaldo ameendelea kujitengenezea rekodi yake mpya kwenye mchezo wa soka.



Alhamisi hii mchezaji huyo alifanikiwa kufikisha goli lake la 500 kati ya mechi 638 wakati Real Madrid ikipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Club America ya Mexico katika mchezo wake wa nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa vya dunia huko nchini Japan.

Magoli hayo yote ni yale aliyofunga akiwa na timu za vilabu pekee, ikiwemo Sporting Lisbon ya Ureno aliifungia magoli matano katika michezo 31, Manchester United alifunga magoli 118 kati ya mechi 292 na timu yake ya sasa ya Real Madrid kashafunga magoli 377katika michezo 366 aliyocheza.

Wakati huo huo Ronaldo ndio mfungaji bora wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Ureno akiwa ameshafunga jumla ya magoli 68 mpaka sasa.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment