Mwanangu akilia huwa namnyamazisha na Muziki ya Darassa – Kala Jeremiah


Hakika Muziki ya Darassa ni ngoma ambayo bado inazidi kufanya vizuri Hapa bongo.



Ukiachia mbali kupendwa tu na mashabiki, hata baadhi ya wasanii wamekiri kuwa wapenzi wakubwa wa wimbo huo uliotoka mwishoni mwa mwaka jana. Kupitia kipindi cha Super Mega cha Kings Fm Radio, rapper Kala Jeremiah amekiri kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa wimbo huo,na hata mwanae pia anaupenda kuliko kawaida.

“Na mimi ni miongoni mwa watu ambao naupenda pia, hata mwanangu anaupenda pia. Mwanangu hata akiwa analia, ukimwekea ule muziki, anafurahi,” amesema Kala Jeremiah.

Kuhusu Ngoma hiyo kuwa na ujumbe, Kala amedai kuwa wimbo huo hauna ujumbe wowote, kitu ambacho amedai hata mwenyewe Darassa anajua kama ngoma yake haina ujumbe.

Na Prince Ramalove – Kings




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment