Hussein Machozi aeleza kisa cha kuyaficha mahusiano yake ya kimapenzi


Hussein Machozi ni msiri mkubwa kwa sasa katika ile sekta mashuhuri ya malavidavi.



Mkali huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akiishi nchini Italia amesema sababu kubwa ya kutoyaweka sana mahusiano yake hadharani ni kutokana na kuamua kuyaweka pembeni na kazi zake.

“Kiukweli ni kwamba yupo, lakini huwa sipendi kuweka mahusiano yangu hadharani. Muziki wangu hauhusiani kabisa na mahusiano yangu. Hayo ni maisha yangu kabisa binafsi,” Machozi alimjibu shabiki kwenye video aliyoiweka Instagram.

“Hata mwenyewe ambaye niko naye huwa hapendi hata kutokea kwenye gazeti, hanaga social network,” aliongeza.

Muimbaji huyo hivi karibuni amepanga kuachia wimbo wake mpya baada ya kuwa kimya kwa muda.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment