AY ataja baadhi ya uwekezaji anaofanya, zimo hisa, nyumba na mashamba



Ambwene Yessayah aka AY hakuitwa Mzee wa Commercial kwa bahati mbaya.





Damu ya kufanya biashara kwenye burudani ilikuwa ikichemka tangu akiwa kidato cha pili pale alipoandaa show ya wasanii wa Dar mjini Dodoma.

Kupitia kipindi cha Chill na Sky hivi karibuni, AY alielezea baadhi ya uwekezaji anaoufanya.

“Kuna vitu vingi,” alisema AY.

“Nawekeza kwenye ardhi, nainvest kwenye hisa, na hizi ambazo nafanya na akila Salama na Josh, Mkasi TV ambamo kuna Siasa za Siasa, kuna Mkasi na kuna vingine vinakuja,” aliongeza.

“Na pia nimeinvest kwenye kilimo [nina mashamba] yapo Ifakara na nataka kutanua zaidi sababu nimegundua ndio mara yangu ya kwanza kufanya kitu kama hiki lakini imenipa msukumo na nitazidi kuiweka iwe kubwa zaidi hadi ifike kwenye heka elfu 10 huko.”

AY alikiri taarifa kuwa ni kweli anajenga nyumba kubwa ya kuishi katika maeneo ya Kigamboni na amesema anataka kuishi kwenye nyumba inayovutia.

“Nina project nyingine ya kujenga kitu kikubwa kwaajili ya biashara, kuna project moja nzuri sana naamini nikiweza kufanikiwa itakuwa moja ya sehemu inayovutia sana.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment