Cpwaa ameiambia Bongo5 kuwa alikuwa amepanga kuachia ngoma mpya mwezi huu lakini ameamua kuahirisha kutokana na hali uchaguzi.
“Kwa sababu sasa hivi masikio na akili ya kila mtu ipo kwenye uchaguzi, sasa ukitoa ngoma haitaenda popote,” amesema. “Hata media zenyewe zipo busy ku-cover uchaguzi na mambo ya kampeni. Kwahiyo muda huu sio mzuri kwangu kwa kuachia nyimbo. Nimeamua niahirishe mpaka baada ya uchaguzi ndio nitaachia ngoma mpya. Ila mwendelezo upo pale pale. Kuna ngoma za aina mbalimbali tayari nimeshaandaa, kuna moja ipo kibongoflava zaidi na moja ipo kimataifa zaidi,” ameongeza.
“Kwahiyo nitangaalia ipi itaenze kutoka na situation ilivyo. Hata kama uchaguzi ukiwa umepita lakini natakiwa kuangalia watanzania wapo kwenye mood gani. Kama ni nyimbo ya mapenzi au nyimbo ya kuruka, au nyimbo ambayo ina ujumbe wa maisha yaani kikubwa zaidi nitaangalia mood ya watanzania.”
0 comments:
Post a Comment