Tuzo kwa mvinyo bora Ufaransa:
Ufaransa inasifika kwa utamaduni wa kutengeneza mvinyo
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaja tuzo hiyo kama kitambulisho cha kimataifa cha torathi za Ufaransa.
Katika kukiri wazi umuhimu wa utamaduni wa kutengeneza mvinyo Ufaransa, UNESCO limetaja mashamba ya zabibu na maghala ya kihistoria ya kutengeneza Champagne Ufaransa kama torathi za kimataifa.
Limesema hadhi hiyo maalum inatolewa kwa maeneo yote mvinyo huo unakotengenezwa kuanzia karne ya kumi na saba kuendelea mbel ikiwemo mashmba ya Reims na Epernay.
Mashamba na maghala ya zabibu Ufaransa yanayotumika kutengeneza Champagne
Katika maeneo yalio na joto kusini magharibi mwa Ufaransa, mashamba ya Burgundy, yanayotumika kutengeneza mvinyo ulio bora duniani aina ya red wine pia yametambulika.
Katika mkutano uliofanyika huko Bonn Ujerumani, UNESCO pia lilitangaza mji wa kale wa Diyarbakir kusini mashariki mwa Uturuki kuwa ia torathi ya kimataifa pamoja na kanisa la Moravian huko Christiansfeld, Denmark.
Hadhi hiyo ya eneo kutangazwa kuwa torathi ya kimataifa huenda ikashinikiza utalii na kuleta faida nyingine za kiuchumi.
Lakini wakosoaji wanasema uharibifu wa maeneo ya kale huko Iraq na Syria yanadhihirisha jinsi UNESCO isivyoweza kuyalinda maeneo yanayopewa hadhi hiyo.
0 comments:
Post a Comment