Bunge la Tanzania lavunjwa rasmi:





Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania hii leo amehutubia rasmi bunge la 10 la nchi hiyo na kulivunja rasmi.

Katika hotuba yake ndefu, rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kuainisha changamoto na mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika uongozi wake kabla ya kuagana na wabunge hao.

Hata hivyo hotuba yake imesusiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani baada ya kulisusia bunge hilo kwa madai ya kupitisha miswada kadhaa bila kufuata utaratibu.

Mnamo mwaka 2010 wakati Kikwete alipokuwa akilifungua bunge la kumi,wabunge wa upinzani walisusia uzinduzi huo pia.

Bunge la Tanzania


Wabunge hao walitangaza kususia Bunge hilo kutokana na uamuzi wa serikali kuwasilisha miswaada mitatu ya mafuta na gesi kwa hati ya dharura.


Pamoja na mambo mengine, Bunge hilo litakumbukwa kwa mjadala mkali uliohusu maamuzi ya sakata ya uchotwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 200 za akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa benki kuu ya Tanzania.


Sakata hiyo liliwaondoa mawaziri wawili na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini na vigogo wengine wa Ikulu ya rais.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment