EU yajadili kukata msaada Burundi

Bendera ya Burundi

Muungano wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi. Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.Federica Mogherini wa EU

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima.

Upande wa uchaguzi ulisusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii.

Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.ghasia katika barabara za Burundi

Ghasia zimezuka nchini humo tangu rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kuwania kiti hicho ambapo zaidi ya watu laki moja wamikimbia nchi hiyo huku makumi ya maelfu wengine wakiuawa katika maandamano.

Juhudi kadhaa za kuleta upatanishi kati ya makundi hasimu zimeambulia patupu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment