Msanii wa muziki anayekuja kwa kasi, Galaxy ambaye video ya wimbo wake mpya ‘Tam Tam’ ilifanyika nchini Uganda, ameeleza kwanini aliamua kutoifanyia nyumbani.
“Nilimua kwenda kufanya nje ya nchi kwakuwa kuna ubora wa video ambao nilikuwa nautaka hasa wa ukanda wa East Africa,” amesema.
“Hii unajua ningeifanyia hapa bongo lakini plan ambayo nilikuwa nimepanga kufanya, nilikuwa kila nikiongea na baadhi ya madirector, walikuwa kama hawanielewi, nikaona nije kujaribu kazi yangu ndio tukawa tumeona kazi ya Chameleone ‘Wale Wale’ tukaona ni nzuri ndio tukaongea naye akasema kuwa anaweza ndio tukaenda kufanya naye hiyo video,” ameongeza.
“Pia sasa hivi najindaa kuachia wimbo wangu mpya, utatoka muda wowote nadhani video nayo nitafanyia nje ya Tanzania, ila bado sijajua itakuwa wapi na director gani, ila mipango ndio hiyo.
0 comments:
Post a Comment