Sijui kwanini watu wamepaniki baada ya kuona mjengo wangu – Linah


Linah Sanga amejikomboa kwa kukaribia kukamilisha mjengo wake japo anadai watu wengi wamekuwa wakijaribu kumkatisha tamaa.


Linah alifanya ukaguzi kwenye nyumba yake inayoendelea kujengwa

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa haikuwa rahisi kujenga nyumba hiyo kutokana na kipato chake kidogo na hivyo kuamua kuijenga taratibu.

“Yeah ile ni nyumba yangu, ipo Mbezi sehemu moja inaitwa Mpiji Magoe,” amesema. “Ile sio nyumba ambayo natarajia nitaishi mimi, nataka kuifanyia biashara halafu nijenge nyingine ambayo itakuwa maalum kwaajili ya kuishi. Naona watu wengi kama wamepaniki, ile nyumba nimejenga kidogo kidogo mpaka pale ilipofika na ikiisha tu ile naanza yangu,” ameongeza.

‘Nimekuwa nikiijenga taratibu, nikipata milioni mbili nanunua tofali mpaka inakamilika. Unajua watu wengi kwenye mitandao wapo kwaajili ya kuku-challenge, mimi ninaweza nikawa nimechukia na kukata tamaA lakini nagundua hawa watu wapo kwaajili ya kutukatisha tamaa. Lakini unaamka na nakusonga mbele nikihakikisha nakipata kile nilichokipanga.”

Kwa upande mwingine Linah amesema ataachia video yake mpya wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment