Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Clara Mwatuka, amefariki dunia kwa ajali




Clara Mwatuka enzi za uhai wake.

Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Clara Mwatuka, amefariki dunia leo Jumapili jioni baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka lilipokuwa linashuka eneo la Makonde Plateu kuelekea Ndanda, Masasi mkoani Mtwara.



Gari alilopata nalo ajali marehemu Mwatuka.
Gari ilikuwa inaendeshwa na dereva wake, ambaye inasemekana ni mwanaye. Maiti ya marehemu Mwatuka imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda. Viongozi waandamizi wa CUF wamethibitisha kutokea msiba huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment