Baada ya Baadhi ya Mashabiki Kumshambulia kwa Maneno, JB Asema Haya


Kufuatia kitendo baadhi ya mashabiki kumshabulia kwa maneno makali staa wa Bongo Movies, JB kwa kuonyesha mapenzi yake kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, JB amefunguka haya kwenye ukurasa wake mtandaoni kuwataka wabadilike kimtazamo.

Hakuna kitu muhimu kwenye maisha kama furaha....lakini furaha ina ambatana na kufanya mambo ambayo moyo wako unapenda bila kuvunja sheria.

Kuishi maisha ya kuogopa kitu unachopenda kwa sababu ya watu ni kuinyima furaha roho yako...watanzania wenzangu tuanze tabia ya kuheshimu maamuzi ya wenzetu.

Angalia hata kwenye mahusiano yetu watu wakiachana ni uhasama..kisa hatukubali kuwa mwenzako moyo wake uko kwingine.

Eti lazima akupende ww tu..haa...kwenye siasa ndio usiseme mtu akipenda upande mwingine ashakuwa adui.Aaah tubadilike.....sambaza upendo..+255 kwanza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment