Ben Pol ashangazwa na club za Kenya kutocheza muziki wa wasanii wao






Miongoni mwa vitu vilivyomshangaza The King Of R&B Bongo, Ben Pol alipokuwa Kenya hivi karibuni ni jinsi muziki wa wasanii wa Kenya usivyopewa nafasi kwenye clubs za huko.



Ben Pol ambaye aliungana na wanamuziki wengine wa Afrika katika msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Afrika jijini Nairobi, alisema kuwa alishangazwa kusikia wimbo mmoja tu wa msanii wa Kenya ukichezwa katika club 4 alizozitembelea kwa usiku mmoja.

Katika kutupa uzoefu wa safari yake ya Kenya, muimbaji huyo wa ‘Sophia’ ametuambia kuwa muziki wa Nigeria, Marekani pamoja na Bongo kidogo ndio aliobahatika kuusikia zaidi katika club hizo.

tumeenda kwenye zile club,tumeenda hapa tumekaa dakika 45 hadi lisaa halafu tunaenda sehemu nyingine hivyo hivyo…sasa ndo nikawa naskia ngoma nyingi zinazopigwa pale ni Nigeria, Marekani na Bongo kidogo lakini husikiii kabisa ngoma za Kenya san asana sijui nilisikia moja tu katika sehemu zote hizo nilizopita.”

Agosti 10 mwaka huu umoja wa wasanii wa Kenya (KENAM) waliandamana katika mitaa ya jiji la Nairobi kudai vituo vya Radio na Televisheni vipige zaidi muziki wao badala ya wa Nigeria, na Agosti 12 serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa ilizindua sera ya taifa ya muziki ambayo inavilazimu vyombo vyote vya habari kucheza muziki wa Wakenya kwa asilimia 60.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment