Mambo 22 usiyoyajua kuhusu Chris Brown (Mpya)

Muimbaji wa Marekani, Chris Brown ambaye yupo kwenye ziara ya ‘One Hell of a Nite Tour’ ameshare mambo kadhaa kupitia mtandao wa Us Weekly ambayo wengi hawayafahamu.

Chris-Brown-PNG

Nayo ni:
1. Ni mtu anayependa sana usafi (neat freak)
2. Ni msanii pekee aliyekuwa jela lakini akawa na wimbo uliokamata nafasi ya kwanza kwenye chart
3. Amejifunza martial arts na masumbwi
4. Anamiliki migahawa 14 inayouza burger na chakula cha haraka (Burger Kings)
5. Alipata tattoo yake ya kwanza akiwa na miaka 13
6. Nyimbo zake zote huzifanya kwa freestyle
7. Hupenda kuchora michoro ya ukutani na fedha zote huzigawa kwenye charity.
8. Hivi karibuni alienda kanisani kwa mara ya kwanza katika miaka 15 na anasema alipenda
9. Ni mpenzi wa vitabu vya katuni
10. Huongoza au hushirikiana kuongoza na kuhariri video zake zote
11. Alimnunulia mama yake nyumba ya dola milioni 1 akiwa na umri wa miaka 15
12. Hali nyama ya ng’ombe wala kitimoto
13. Huzungumza na mchungaji mara mbili kwa wiki
14. Alipokuwa na miaka 6 alimshuhudia ndugu yake akijaribu kujiua
15. Ni mtu mwenye hisia sana
16. Gari lake la kwanza kumiliki lilikuwa ni Lamborghini
17. Anasema hutabasamu mara nyingi kwasababu anaamini dunia hairuhusu watu kulia
18. Alipoanzisha brand yake ya nguo aliingiza faida ya dola milioni 4 kwenye mwaka wake wa kwanza
19. Anapenda kucheza na mwanae wa kike [Royalty, miezi 15].
20. Anapenda kumchagulia binti yake nguo za kuvaa
21. Anasema mafanikio na fedha hazijawahi kumbadilisha
22. Anasema kitu bora kabisa Mungu amewahi kuumba ni mwanamke


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment