Davido, Wizkid wafungiwa
SHIRIKA la Utangazaji nchini Nigeria (NBC), limetangaza kuzifungia nyimbo mbalimbali zisizo na maadili, zikiwemo za wasanii nyota wa nchini humo, Davido na Wizkid.
Wimbo wa Davido uliotangazwa kufungiwa ni ‘In Do Me’ na wimbo wa Wizkid uliofungiwa ni ‘In My Bed’, nyimbo hizo zimefungiwa kupigwa kwenye vituo vyote vya runinga na radio nchini humo kutokana na kukosa maadili kwa jamii.
Nyimbo nyingine ambazo zimefungiwa kupigwa kwenye radio na runinga nchini humo ni pamoja na wimbo wa Nicki Minaj ‘Anaconda’, Ace Hood ft Rick Ross ‘Bugati’, May D ‘Ibadi’, Iyanya ft Don Jazzy ‘Gifts’, Omarion ft Chris Brown ‘Post To Be’ na nyingine nyingi.
0 comments:
Post a Comment