Mo Music amtamani KCEE katika wimbo wake mpya


BAADA ya wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva kufanya vizuri kimataifa kupitia ushirikiano na wasanii wa kimataifa, msanii anayefanya vizuri katika wa muziki huo, Moshi Katemi ‘Mo Music’ naye ana matarajio ya kushirikiana na msanii kutoka Nigeria, KCEE.

Mo Music, anayetamba na wimbo wa ‘Basi Nenda’ na ‘Ntazoea’, alisema ameshafanya mawasiliano na msanii huyo na mipango ikienda kama walivyopanga watakamilisha wimbo huo ndani ya mwaka huu.

“Nimemchagua KCEE kwa sababu nakubali kazi zake, lakini pia atanisaidia kibiashara na kunitangaza kimataifa,” alisema Mo Music.

Msanii huyo asiye na ndoto ya kutoa albamu katika maisha yake ya muziki aliwataka wasanii wenzake kuachana na masuala ya ushabiki wa timu, badala yake waungane ili wawe na nguvu moja ya kutangaza muziki wao ndani na nje ya nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment