Tukio hilo lilitokea jana mchana kwenye kipindi cha XXL ambapo mtangazaji wa kipindi hicho, Bdozen alitaka kujua kwanini wawili hao hawaelewani. Diamond alidai kuwa Diva amekuwa akimuongelea vibaya kwenye kipindi chake.
“Mimi nimewahi kukuzungumzia vibaya where,” Diva alimuuliza Diamond. “Unazungumza vibaya sana,” alisema Diamond na kuongeza, “Tatizo na mimi mpaka najilaumu labda ningekuwa nimekukaza usingekuwa unaniongelea hivi, I am telling you.” “You are not my type, hauwezi kunikaza,” alijihami Diva.
Diva ameiambia Bongo5 baada ya majibizano hayo, Diamond alinyanyuka alipokuwa amekaa kutaka kumpiga lakini watu waliokuwemo ndani ya studio hizo walimzuia.
“Amenidisrespect, amenidhalilisha kama mwanamke,” amesema Diva. “ Evidence is everywhere, the clip is going viral na inaniaffect mimi as a woman, inaniletea mateso in my life right now. Alinitukana, alinitishia kunipiga mpaka aliposhikwa na wenzie,” anasema mtangazaji huyo.
“Kwahiyo hiyo issue ipo kwa mwanasheria wangu, they are working on it.”
Kuhusu kama uongozi wa Diamond umechukua juhudi za kuwasiliana naye ili wayamalize Diva amesema: Uongozi wake uliandika kwenye Twitter kuwa nipeleke malalamiko yangu sehemu husika. Kwahiyo kama mtu anapata guts za kukusdisrespect, anakudhalilisha, anakutishia maisha and all that na management yake inakuambia kalalamike sehemu husika, nimewaambia note I will do that.”
Diva amedai kuwa kinachomuuma zaidi ni mashabiki wa Diamond ambao wanamtukana matusi ya kila aina kwenye Instagram.
“My dad, mama yangu amefariki wanamtukana matusi, inauma. Sina moyo wa chuma mimi, I am human.”
Uongozi wa Diamond umeiambia Bongo5 kuwa hawatishiki na uamuzi wa Diva na kusisitiza kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimchafua staa huyo wa ‘Nana’ mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment