Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz soko la muziki wa Uganda ni imara na linalipa zaidi kuliko la Tanzania.
Ommy Dimpoz akiwa na msanii wa Uganda, Eddy Kenzo.
Ommy amedai kuwa mwaliko wake wa kwenda kutumbuiza kwenye show kubwa ya mshindi wa tuzo za BET mwaka huu, Eddy Kenzo kumemfumbua macho. Amedai kuwa wasanii wa Uganda wanapata support kubwa kutoka kwa makampuni na mashabiki kuliko wasanii wa Tanzania.
“Nilichogundua ni kwamba support ni kubwa sana, kuanzia kwa mashabiki mpaka kwa makampuni,” Ommy ameiambia Bongo5.
Akitolea mfano tamasha la Eddy Kenzo, Mbilo Mbilo concert, Ommy amedai kuwa makampuni mengi makubwa yalilidhamini kwa kutoa fedha nyingi na hivyo msanii huyo kuingiza fedha nyingi hata kabla ya show yenyewe.
Ommy Dimpoz akiwa na msanii wa Kenya, Amani ambao wote walialikwa kwenye show ya Eddy Kenzo
Kingine amedai kuwa tamasha hilo lilifanyika kwa siku tatu mfululizo ndani ya jiji la Kampala lakini kwenye viwanja tofauti na vyote vilijaa.
“Zilifanyika show tatu na zote sold out,” amesema.
Ommy aliyetumbuiza hits zake karibu zote kwenye show hiyo amedai kuwa kilichomvutia kingine ni show hiyo kuanzia mapema na kumalizika mapema tofauti na za hapa kwetu ambazo huisha alfajiri. Amedai kuwa kuwa show ilianza saa tatu usiku na kumazika saa sita usiku.
Eddy Kenzo alitumbuiza kwa live band na Ommy amedai uwezo wa bendi hiyo na vyombo vilivyofungwa ulifanya muziki usikike kama unapigwa kutoka kwenye CD!
0 comments:
Post a Comment