Feza Kessy kufanya muziki na Sauti Sol, Mafikizolo na Ali Kiba, Msikilize hapa



Staa wa muziki Feza Kessy, ambaye hivi sasa amezindua track ambayo ni kolabo yake na Chegge ya 'Sanuka', amefarijika kutumbuiza katika onesho kubwa la muziki la Party In The Park lililofanyika jijini Dar.

Katika onesho hilo lilokusanya maelfu ya mashabiki na mastaa mbalimbali, pamoja na kutumbuiza vyema stejini Feza aliwamwagia sifa wanamuziki Sauti Sol, Mafikizolo na Ali Kiba ambao walitikisa na muziki wao wa Live.

Feza ameiambia enewz kwamba amegundua kuwa kitu ambacho kinawafanya wasanii hawa nyota kuzidi kutambulika kimataifa ni kwa sababu ya kubakia katika asili yao kisanaa na hii ni kutokana na kujituma zaidi ili kufikia malengo yao kimuziki.


Aidha Feza amesema kwamba mipango yake ikikaa sawa anatarajia kufanya kazi na nyota hao ambao kwa kiasi kikubwa amevutiwa nao sana, huku akifurahi kuona wimbo wake wa 'Sanuka' kupokelewa vyema na mashabiki wake akisema 'the future for Feza is brighter than bright, Watch Out world.
Endelea kutazama EATV ambapo tutaendelea kukujulisha yaliyotokea katika onesho hilo lililofanyika wikend iliyoisha pale The Green Oysterbay Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam, tukiwa moja ya wadhamini wa nguvu kabisa wa burudani hiyo ya kukata na shoka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment