Wasanii wa Tanzania kulipa Tsh Milioni 4 ili kupewa kibali ili kufanya show Mombasa


Gazeti la The Star la Kenya limeripoti kuwa wasanii kutoka nje ya Mombasa watakaoenda kufanya maonesho mjini humo, watalazimika kulipa kiasi kikubwa cha pesa ili kupewa kibali.

Gazeti hilo limemnukuu Gavana wa Mombasa akisema kuwa , wasanii kutoka mikoa mingine nje ya Mombasa ikiwa ni pamoja na wale wa Nairobi , watalazimika kulipa shilingi ya Kenya 200,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 4 ya Tanzania ili kupewa kibali cha kutumbuiza.

“Ni lazima tujivunie wasanii wetu, msanii yeyote atakayetaka kufanya onesho Mombasa kutokea mikoa mingine ikiwemo Nairobi watatakiwa kulipa sh 200,000 kwetu kabla hawajapewa kibali cha kufanya onesho au nyimbo zao kuchezwa kwenye club za hapa.” Amesema Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Ameongeza kuwa vituo vya Radio, Tv na club hazitacheza nyimbo za wasanii kutoka nje ya Mombasa mpaka pale watakapolipia kiasi hicho kwa Serikali ya County ya Mombasa.

Joho amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa ili kusaidia kukuza vipaji vya wasanii wa Mombasa.

Kudhihirisha kuwa County ya Mombasa ina dhamira ya dhati kuhusu uamuzi huo, Afisa wake wa Vijana, Michezo na Utamatudi , Mohamed Abass, amesema kuwa maelekezo hayo yatajumuishwa katika muswaada wa fedha wa County ya Mombasa 2015-2016.

Hatua hii itawagusa sio tu wasanii wa Nairobi na mikoa mingine Kenya, lakini hata wasanii wa Tanzania ambao wamekuwa wakipata mialiko mingi ya kufanya maonesho Mombasa.

Nini maoni yako katika hili?
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment