Christian Bella akiwa kwenye gari yake mpya
Akizungumza na Bongo5 leo akiwa mwenye furaha, hitmaker huyo wa Nani Kama Mama amesema bado anatamani kuwa na magari mengi zaidi na ya thamani.
“Mimi napenda sana kuwa na magari mengi ndio maana nikipata pesa na gari nikilitamani nalinunua tu,” amesema. “Tatizo ni pesa, leo gari yangu mpya imeingia Toyota Harrier. Hii gari niliagizia ndio imeingia, nimenunua shilingi milioni 35.”
0 comments:
Post a Comment