Kundi la P-Square kutoka Nigeria linaendelea kuvunja rekodi waliyoiweka wenyewe kupitia video ya hit single yao ‘Personally’.
Rekodi mpya ilivyowekwa na Peter na Paul Okoye wa P-Square, wamekuwa wasanii wa kwanza kutoka Afrika kufikisha views milioni 50 kwenye mtandao wa Youtube kupitia video ya ‘Personally’, .
November 2014, P-Square waliweka rekodi kwa mara ya kwanza kwa kuwa wasanii wa kwanza Afrika kufikisha views milioni 30 Youtube kupitia video hiyo.
April 2015 kundi hilo lilivunja tena rekodi yao wenyewe baada ya video hiyo kufikisha views milioni 40.
Na sasa tena video hiyo iliyotoka June 21, 2013 imekuwa video ya kwanza ya msanii wa Afrika kufikisha zaidi ya views milioni 50. Video ya ‘Personally’ iliongozwa na kaka yao Jude Engees Okoye.
Jikumbushie kwa kuitazama hapa:
0 comments:
Post a Comment