Kwa mujibu wa TMZ, flamu nyingine itakuja itakayoangalia maisha ya Snoop Dogg, Tupac na rappers wengine wa West Coast.
Rapper wa Dogg Pound, Daz Dillinger ameuambia mtandao huo kuwa filamu hiyo itaanzia pale N.W.A. ilipoishia na kuangalia maisha ya Snoop, Nate Dogg, Kurupt, Daz na Warren G. Filamu hiyo itaitwa ‘Dogg Pound 4 Life.’
Inadaiwa kuwa mtoto wa Dr. Dre, Curtis Young, ataigiza nafasi ya baba yake. Bado hakuna mtu aliyefahamika atakayemuigiza Snoop na Ice Cube japo waigizaji hao hawatakuwa wale wale waliogiza kwenye filamu ya ‘Compton.’
Dre na Cube hawataitayarisha filamu hiyo lakini Daz anadai kuwa Cube ameibariki.

0 comments:
Post a Comment