Hakuna dalili ya kumalizika karibuni beef kati ya 50 Cent na P.Diddy ambayo imekuwepo kwa miaka mingi.
Curtis James Jackson III a.k.a 50 Cent kwa mara nyingine amemchokoza mpizani wake Diddy, kwa kupost picha akiwa na mzee na kumkejeli kwa kuandika caption kana kwamba huyo mzee ndio Diddy.
“Mimi na Puff tukiwa tumekaa leo alisema, 50 ninazeeka sasa, mimi nikasema najua” na mwisho akamalizia kwa emoji ya kicheko iliyofatiwa na hashtag ya kinywaji chake #Effenvodka ambacho pia ni miongoni mwa vitu vinavyowafanya Diddy na Fiddy wawe wapinzani wa kibiashara, sababu Diddy naye ana kinywaji cha Ciroc vodka.
0 comments:
Post a Comment