Mwasiti awashauri wananchi kuwa makini na sheria ya makosa ya mtandaoni

Muimbaji wa Nalivua Pendo, Mwasiti Almas amesema anaisubiria kwa hamu sheria mpya ya makosa ya mtandaoni itakayoanza kutumika September 1 mwaka huu.

Mwasiti

Akizungumza na Bongo5 leo, Mwasiti amewataka wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kuwa makini na sheria hiyo.
“Hii sheria itapunguza maudhi ya kwenye mitandao,” amesema. “Watu wengine wanaogopa kuingia kwenye mitandao kwa sababu ya kutukanwa. Watu watakuwa huru zaidi. Kwa wasanii na watanzania ambao hawaweki ujinga itakuwa ni vizuri lakini kwa wale wanaotumia mitandao kama silaha yao watakoma, Itawafanya waogope,” ameongeza.
“Kiukweli mimi nimefurahi sana, kwenye mtandao watu wanaweza wakakufanya mpaka ujione sio binadamu, kumbe na wewe una nafasi yako kubwa sana na ninaisubiria kwa hamu kubwa sana na itanyoosha watu na watu wataheshimu mitandao kama wanavyoheshimu sehemu nyingine.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment