Professor Jay asema akiwa mbunge asitegemewe sana kuongelea matatizo ya wasanii

Wasanii wasitegemee msaada wa maana pindi Professor Jay akiingia bungeni. Rapper huyo anayewania ubunge kwenye jimbo la Mikumi mkoani Morogoro amesema atatumia wadhifa huo kuwahudumia wananchi wa Mikumi.


Professor amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi hivyo atatumia muda kuwatumikia watu wake.

“Nimewaambia wasanii wangu na wanajua nimechaguliwa kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo la Mikumi, lakini wengi wamesema watanisaidia kwa maneno lakini bado sijalaunch kampeni yangu rasmi. Natarajia kulaunch natarajia rasmi tarehe 5 mwezi wa tisa, sasa tunaangalia nani atani-support,” amesema.

“Mimi ni kijana na mimi ni mwanamuziki, watu waelewe naingia bungeni kwenda kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Mikumi, kwahiyo tutafanya kazi sawa za wananchi wa jimbo la Mikumi na Professor atakuwa anaishi Mikumi na nitakuwa napatikana huko Mikumi.”

“Watu wasitegemee nitaingia bungeni kwenda kuongea masuala ya wasanii sana kuliko hata kuwawakilisha watu wa Mikumi. Watu wajue Professor Jay atakuwa mbunge wa watu wa Mikumi ni vile ni mwanamuziki nitapigania kwa hali na mali maslahi ya muziki ili kuweka sanaa katika level za juu zaidi.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment