Muimbaji wa Marekani, Taylor Swift anadaiwa kuipiga chini dili ya kutumbuiza nyimbo 3 tu kwenye harusi ya bilionea mmoja, ambayo ingemuingizia dola milioni 2, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 4.
Inasemekana kuwa Taylor alifanya uamuzi huo wa kuipotezea dili hiyo ili ahudhurie na kutumbuiza bure kwenye sherehe ya ubatizo wa mtoto wa rafiki yake aitwaye Jaime King huko Los Angeles, Marekani. Hii ina maanisha kuwa dili hiyo pamoja na sherehe ya rafiki yake vilidondokea siku moja hivyo alilazimika kuchagua kimoja.
“You have to admire her for putting friendship ahead of financial considerations. She said no to a small fortune so she could bring happiness to a good friend.” – mmoja wa waliohudhuria sherehe hiyo aliliambia gazeti la Sunday Express.
Taylor alihudhuria sherehe hiyo akiwa na boyfriend wake Calvin Harris.
Taylor na Calvin mwaka huu walitajwa na jarida la Forbes kuwa couple maarufu iliyoingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2015, na kuwazidi Jay Z na Beyonce waliokuwa wamekamata nafasi hiyo mwaka uliopita. Kwa pamoja waliingiza dola milioni 146.
Hii inaonesha kuwa Taylor hana njaa, na huenda hiyo ni sababu ya kuamua kumjali rafiki yake badala ya dola milioni 2 za bilionea aliyemtaka akatumbuize kwenye harusi yake kwa muda mfupi.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment