Abdul Kiba kuja na kolabo na msanii wa Nigeria

Abdul Kiba amesema tayari ameshaanza kufanya mazungumzo na wasanii wa muziki kutoka Nigeria ili kukamilisha kolabo yake.

11850188_1690024774564223_162750966_n

Msanii huyo ambaye ni mdogo wake na Ali Kiba, ameiambia Bongo5 hivi karibuni kuwa lengo lake ni kuhakikisha na yeye anafanya vizuri kimataifa.

“Tayari nimeanza mazungumzo ya kolabo na wasanii wa Nigeria ili kutanua wigo wangu wa muziki,” amesema. “Kila kitu hapa ninapozungumza kinaenda vizuri, siwezi kuwataja ni akina nani lakini nimezungumza nao. Ni wasanii wakubwa na nikifanya nao kazi zitakuwa na impact katika muziki wangu. Tayari nimeshawatumia kazi nasubiria wapokee audio zangu ili tujue ni lini kazi zinaanza,” ameongeza.
Kiba ameeleza kuwa kufanya kolabo na wasanii wa Nigeria kuna faida kwakuwa ni wasanii ambao muziki wao unafanya vizuri katika kila kona ya Afrika kwa sasa.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment