Vanessa Mdee awashauri wasanii wasiogope kufanya matamasha kipindi hiki kwa kuhofia uchaguzi


Vanessa Mdee

Vanessa Mdee amesema kuwa wao hawaoni sababu ya kuogopa kuendelea kufanya kazi zao hata katika kipindi hiki kwasababu hiyo ndio kazi inayowapa kipato.
“Kusema kweli tunathubutu kufanya show kipindi cha uchaguzi kwasababu kwetu muziki ni ajira ni kazi yetu…Hatuwezi kusitisha kile ambacho kinatuletea mkate,” alisema Vanessa kupitia 255 ya XXL.

good music
Good Music family wakiwa Mbeya

Vee Money hakusita kuwashauri wasanii wengine ambao wamesitisha kufanya kazi zao katika kipindi hiki cha uchaguzi.
“Ningewasihi wasanii wengine wasiogope kufanya vitu katika kipindi hiki kwasababu kama ni ajira yako hutakiwi kuacha kufanya katika kipindi hiki, kitu kikubwa zaidi siku ya kupiga kura wote tuunganike kama Watanzania tukapige kura.”
Kupitia Instagram Jux pia alishare picha na kuonesha kinachoonekana kuwa mavuno ya show ya Mbeya na kuandika:
Jux mbeya

“Asanteni mbeya kwa upendo wenu #africanboy I ain’t walking for no cheesecake #mbeyamoney #goodmusicfamily we coming to your city soon”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment