Ben Pol aipiga chini management ya Panamusiq



Ikiwa ni miezi 5 tu imepita toka Benard “Ben Pol” Paul atangaze kusaini mkataba wa usimamizi na kampuni ya Panamusiq, mwimbaji huyo wa R&B amevunja nao mkataba.



Bongo5 imemtafuta Ben Pol ili kuzungumzia sababu za kusitisha mkataba huo ambao wakati wanasaini walisema ungekuwa ni wa muda mrefu.

“Unajua tumeanza kufanya kazi mwezi wa 4 na tumeachana mwezi wa 9” alithibitisha kusitisha mkataba.

Ben Pol amesema kuwa kwa kipindi cha miezi 5 ambacho amekuwa na kampuni hiyo kuanzia mwezi April hadi September 2015 alipousitisha mkataba, amekuwa akiweka rekodi ya utendaji na kwa namna fulani kuna vitu ambavyo hakuridhishwa navyo japo hakutaka kuweka wazi sababu halisi ya kusitisha mkataba.

Ameongeza kuwa alikaa mezani na kampuni hiyo na pande zote mbili wakakubaliana kusitisha kufanya kazi, na kuwa wameachana kwa uzuri. Pia amesema wamekubaliana kutotoa tamko rasmi wala kuzitaja sababu za kuachana.

Alhamisi ya wiki hii (Sept 24) Ben Pol ataachia single mpya ‘Ningefanyaje’ aliomshirikisha Avril wa Kenya.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment