Akiongea kupitia kipindi cha The Beat cha NTV ya Uganda Ijumaa iliyopita, Bobi Wine amesema kuwa kazi yake ni kufanya muziki kwaajili ya mashabiki wake wa Uganda, na endapo mashabiki wa nje watapenda kazi hizo ni sawa, lakini haimaanishi kuwa ana mpango wa kufanya muziki kwaajili ya mashabiki wa nje.
Kauli hiyo inakuja kipindi ambacho mastaa wa Uganda kama Jose Chameleone, Bebe Cool, Eddy Kenzo na wengine wanafanya vizuri na kutajwa kuwania tuzo mbalimbali kubwa za kimataifa.
0 comments:
Post a Comment