CCM Wako Bize Wanamsema Lowassa Badala ya Kuwaambia Wananchi ni Lini Watawaondoa Katika Maisha ya Ufukara





Nilidhani watanzania (wapiga kura) walitaka kusikia zaidi ni kwanini wao ni masikini ilhali nchi hii ina rasilimali za kuwafanya waishi maisha bora. Serikali ya awamu ya 4 ilikuja na slogan "Maisha bora kwa kila mtanzania". Katika ziara za wagombea urais Nchi imezungukwa na nyumba nyingi za nyasi yani kwa kifupi bora hata yale mahema ya muda ya wakimbizi. Unawasikia mapambe wa mgombea urais wa CCM wako bize wanamsema ENL badala ya kuwaambia wananchi ni lini watawaondoa katika maisha ya ufukara. Ni ajabu sana kuanzia rais wa awamu ya 4, wapambe kasoro mgombea urais wote hofu yao ENL wakati wao ndio walio madarakani na wanaweza pia kutumia sheria zilizopo kutaifisha wanachohisi si halali yake. Iweje washindwe leo aweze wa awamu ya 5? Iweje Chama hicho hicho kijinandi kitaweza na akijaweza kupambana na mafisadi?

Iweje Chama hicho hicho kinajinadi kitageuza uchumi wa nchi hii kuwa wa viwanda wakati kilimo kwanza kimeshindikana?(yaani uchumi wa raw materials), iweje Wanachama hao hao waendelee kupiga kelele wakiwatolea wapinzani kashfa wakati wao ndiyo wazazi wa mafisadi? Inaniwia vigumu kuielewa CCM na viongozi wake na pengine kukiamini chama hicho kwani ni chama kinachowataka watanzania kuwa watu fukara hata baada ya miaka 53 ya unyonyaji wa haki, kodi na mali zao. Wameshindwa kabisa kueleza ni vipi watatuondolea umasikini. Badala yake wanatoa majibu mepesi ya tutatoa elimu bure mpaka form 4, tutatoa milioni 50 kwa kila kijiji (Tafakari kijiji kina watu 15,000 ina maana mtauondoa umasikini kwa kila mmoja kupata shilingi 3,333/-? acheni masihara. ## Tafakari chukua hatua##

By Philip Mlay
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment