Cliff Mitindo asema angeacha muziki kama haulipi



Rapper Cliff Mitindo amesema kama muziki wa Hip Hop ungekuwa haumlipi angekwisha achana nao.



Cliff aliyepo kwenye maandalizi ya video ya wimbo wake mpya, ‘Natamani’, ameiambia Bongo5 kuwa anaona muziki wake una nafasi kubwa katika soko la muziki hapa nchini.

“Unajua soko la bidhaa kadhaa, kila bidhaa ina watu wake,” amesema. “Kiukweli muziki wa Hip Hop unafanya vizuri sana, pia kwa upande wangu ndio maana naendelea kufanya. Mimi sioni ubaya wa muziki wa Hip Hop sokoni, mimi sioni mabadiliko yoyote kama watu wasemavyo.”

“Kama muziki wa Hip Hop ungekuwa haulipi mimi ningekuwa nimeshaacha, kwa sababu mimi nafanya kwa mapenzi na jinsi ninavyoona faida yake, muziki wa Hip Hop unapendwa sana hata kwenye show tunazofanya ukiangalia unajua muziki wa Hip Hop una nafasi gani kwa jamii.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment