Tamasha la mara pili la kila mwaka, Africa On The Square linatarajiwa kufanyika October 10 na kukutanisha wasanii kutoka Tanzania, Ghana na Senegal.
Tamasha hilo lililoanzishwa mwaka jana na kuvutia watazamaji zaidi ya 20,000, litafanyika Trafalgar Square jijini London, Uingereza.
Pamoja na muziki wa Kiafrika utakaochezwa live, kutakuwepo pia na Madj, dancers, chakula na mambo mengine.
Wasanii wa Tanzania watakaotumbuiza ni Saidi Kanda na Mvula Mandondo watakaotumbuiza muziki wa Kitanzania wenye asili ya kimanyema na kindengeleko.
0 comments:
Post a Comment