Kwa wasanii kuwa maarufu, Wapo wanaojulikana kwa kuwa na sauti ya pekee, kipaji halisi naperformance. Wakati mwingine anapata umaarufu kwa kujulikana kwenye nchi atokayo, huku mwingine akijitengenezea jina lake mwenyewe kupitia utandawazi. Wapo wasanii maarufu ulimwenguni wakike wengi ambao wapo chini ya management nzuri, ila wapo wanao ingiza mkwanja zaidi. Hii ni Top 10 yetu.
Hiyo ilikuwa Top 10 yetu ya wanamuziki wa kike ulimwenguni wanao ongoza kwakulipwa mkwanja mrefu. Wengine labda hata ulikuwa hauwafahamu. Nishushie comment yako next time nije na Top 10 ya nini!
10. Lady Gaga (net worth: $220 Million)
Ana vituko na skendo ila anapata mkwanja mrefu katika wanamuzi wakike ulimwenguni. Mimbaji huyu wa Marekani alipata kuu album yake kwa dola milioni 28 na nyimbo zake kuuzwa kwa zaidi ya dola milioni 140 za Kimarekani.09. Cher (net worth: $305 Million)
Muigizaji, Mwanamuziki na Mwana mitindo kutoka Marekani, Staa anayejulikana kwa sauti ya pekee ambaye ametunzwa jina la 'Goddess of Pop', Amekuwa akitawala moyo wa mwanamke nakusababisha ngoma zake ziwaguse wanaume. Ni mwanamuziki wakike wapekee amaye amezidi kushikilia nafasi kwenye chati ya Billboard.08. Jennifer Lopez (net worth: $315 Million)
Sio kwa uimbaji tu, Ni mwanamke mrembo na mwenye mvuto ambaye wengi wanatamani kuwa na mwanamke kama J Lo. Ni mwanamuziki na Muigizaji maarufu duniani, Kasahuza zaidi ya records millioni 55 ulimwenguni hadi sasa. Ni moja kati ya wasanii ambao pia ni wajasiriamali.07. Barbra Streisand (net worth: $340 Million)
Amekuwa kati ya wasanii bora ulimwenguni kutoka Marekani katika kuuza albumu za musiki wao. Ameshinda tuzo mbili za Academy, Tano za Emmy na tuzo nane za Grammy. Akiwa ameuza zaidi ya album millioni 72.5 Marekani na milioni 245 ulimwenguni.06. Shania Twain (net worth: $350 Million)
Mmoja kati ya wanamuziki wa kike ambaye anapendwa ulimwenguni. Kwasauti yake murua ambayo inavutia ameingiza mkwanja mrefu kutokana na show anazo zifanya na anakimbiza katika uuzaji wa album zake ulimwenguni.05. Dolly Parton (net worth: $450 Million)
Tukija kwenye nyimbo za 'Country' swawia hakuna mwanamke mwingine ambaye atakugusa zaidi ya Dolly Parton. Kwa mkwanja wa dola milioni 450 amekimbiza katika chart za nyimbo za country kwenye Billboard. Amebahatika kuchukua tuzo 7 za Academy na 8 za Grammy.04. Mariah Carey (net worth: $535 Million)
Moja kati ya mwanamuziki ambaye ni kipenzi cha wengi, Mariah Carey ameuza zaidi ya records milioni 200 ulimwenguni. Kwa tuzo za Billboard na Grammy zinathibitisha mwanamama huyu kuwa anakimbiza kwa kuwa na msahabiki.03. Beyoncé (net worth: $536 Million)
Beyoncé ni mwanamuziki wa Rn'B kutoka Marekani, Pia ni muigizaji na mbunifu wa mitindo. Urembo na Kipaji cha pekee kimemsababisha auze zaidi ya ngoma milioni 75 napia zaidi ya ngoma za kundi lao la Destiny's Child milioni 60. Mbali na kazi zake nzuri ametajwa kuwa mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni kwamujibu wa TIME.02. Celine Dion (net worth: $700 Million)
Kunasababu ya yeye kuwa mwanamuziki wa pili ulimwenguni kuingiza mwanja mrefu, Sio kwa pesa tu anazoziingiza bali muimbaji huyu ana kipaji cha kuimba. Ametikisa ulimwengu kwa miondoka ya Rock na Rn'B kwenda kwenye nyimbo za Injili na Classical, Kipaji chake hichi za kuchanganya kimetikisa German, Latin, Japan, Ital hata Mandarin China na dunia kwa ujumla.01. Madonna (net worth: $800 Million)
Madona ameshauza nyimbo zake binafsi 'solo' zaidi ya milioni 300 ulimwenguni kitu ambacho kimempelekea aitwe 'The Queen of Pop'. Ameweka heshima kwenye Guinness World Records kwakuwa mwanamke wapekee kuuza ngoma yake ulimwenguni. Ameshauza hadi sasa zaidi ya album milioni 64.5 ulimwenguni.Hiyo ilikuwa Top 10 yetu ya wanamuziki wa kike ulimwenguni wanao ongoza kwakulipwa mkwanja mrefu. Wengine labda hata ulikuwa hauwafahamu. Nishushie comment yako next time nije na Top 10 ya nini!










0 comments:
Post a Comment