Nyumba 1000 zimeteketa kwa moto uliowaka kwa zaidi ya wiki moja California nchini Marekani



Nyumba 1000 zimeharibiwa na moto ambao umekuwa ukiwaka kwa zaidi ya wiki moja California nchini Marekani.

Maafisa wa idara ya usalama wa umma Kaskazini mwa jimbo la California nchini Marekani wanasema kuwa moto huo huenda ukaenea zaidi na kusababisha uharibu mkubwa zaidi. Takriban watu 5 wameaga dunia kutokana na moto huo.

Idara ya kupambana na majanga imeonya kuwa moto huo umesambaa katika eneo kubwa lenye mamia ya kilomita mraba na huenda watu wengi zaidi wakalazimika kuhama makwao.

Maafisa wanasema kuwa moto wa kipindi hiki katika jimbo la California ambao mara nyingi hutokea kati ya mwezi Septemba na Oktoba unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi katika historia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment