Je unajua fursa zilizojitokeza kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka huu?


Watu wengi tunachukulia kampeni za uchaguzi katika sura mbalimbali. Viongozi wanatafuta nafasi za kupata madaraka kwa gharama yoyote. Na wananchi wanataka viongozi na kati ya wananchi na viongozi kuna madalali na wafanyabiashara.




Dalali kazi yake ni kumsaidia mgombea kupata huduma za kujitangaza na kuendesha kampeni zake na wakati huo huo mfanyabiashara anafanya kazi na dalali wa vyama hivyo hivyo. Mfanyabiashara wakati wote anatafuta biashara mahali popote, inawezekana wakati huu hukuweza kushitukia fursa ukawekeza kwenye mijadala ya kisiasa badala ya kutafuta fursa za kibiashara.

Suala ni kwamba fursa zilizopo kwa sasa inategemea sana wewe ulichukulia uchaguzi kwenye mfumo gani? Ulichukulia kisiasa zaidi au kutafuta fursa zaidi ya kufanya biashara? Kuna watu ambao huwa huwezi kupata fedha yao kirahisi na kama wanasiasa na fedha yao inapatikana wakati wa uchaguzi kama mwaka huu.

Matangazo ya kwenye magazeti, mitandao ya kijamii, redio, vipeperushi na mabango ya barabarani. Wamiliki wa biashara hizo kwa sasa wao ndio wako kwenye mavuno makubwa kibiashara na wale ambao waliweza kuona mapema walianza kutengeneza pesa mapema zaidi. Usishangae kuna watu hata kama wasipofanya biashara miezi sita baadaye baada ya uchaguzi bado watakuwa wako kwenye hali nzuri kwa sababu miezi hii ya kampeni wanaingiza pesa kila siku.

Wana habari nao wanaandika habari zinazovutia wasomaji kisiasa. Si wakati wote utapata habari unayotaka ila ni ile yenye mvuto zaidi ndio itakayouza hata kama haina kitu. Hivyo basi wakati wewe unatafuta kiongozi na wengine wanatafuta wasomaji kama wewe ili wapate kula mkate wao wa kila siku.

Vyombo vya muziki. Wamiliki wa vyombo vya mziki ambao husubiri matamasha ya muziki wa kawaida na kidini kwa sasa wana uhakika wa kupata biashara kila wiki kama si kila siku. Kuna wale ambao bahati iliwakuta vyombo vyao vimechukuliwa na wanasiasa kwenda kusaka wapiga kura huko mikoani na kuna wengine wanakula kidogo kidogo kwa wabunge na madiwani.

Wauza fulana na waweka chapa katika fulana za vyama, nao wamepata bingo. Kundi hili nalo linaendelea kupata ahueni kwenye wakati huu wa kibiashara kwao kuliko hata unavyofikiri. Je unajua fulana zinazouza zaidi msimu huu? Je wewe ulikuwa wapi au uko wapi?

Kwani wewe ulichukulia kampeni kwenye mtazamo gani? Kila jambo linapotokea kuna watu wanafaidika kwa nmna moja ama nyingine awe yuko upande unaoamini utashinda au tofauti na wewe ila kwake muhimu ni kwamba biashara itafanyika na faida lazima ipatikane.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment