Rapper wa Afrika Kusini, K.O ambaye wiki iliyopita alikuja nchini na kufanya media tour, amezungumzia mipango aliyonayo kwa zile collabo anazotarajia kufanya na wasanii wa Bongo.
K.O ambaye ameshirikishwa na Vanessa Mdee kwenye ‘Nobody But Me, amesema kuwa kama mipango ikienda vizuri angependa zile nyimbo atakazofanya na wasanii wa Tanzania kwa kuwashirikisha au kushirikishwa angependa kuzijumuisha kwenye album yake ijayo ya mwaka 2016.
Collabo ambayo tayari ameithibitisha ni ya yeye na Joh Makini, tayari wameingia studio kwa Nahreel kufanya mdundo na kinachosubiriwa kwa sasa ni kila mmoja kurekodi verse zake.
Hii ni hatua kubwa kwa maendeleo ya muziki wa Tanzania pale collabo za wasanii wetu wanazofanya na wasanii wa n je na kuwekwa kwenye album zao ni kitu kikubwa. Iyanya pia ameuweka wimbo aliomshirikisha Diamond ‘Nakupenda’ kwenye album yake mpya iliyotoka hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment