K.O awasifia Nahreel, Diamond






RAPAwa Afrika Kusini, Ntokozo Mdluli, ‘K.O’ amewamwagia sifa nyingi prodyuza, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na msanii wa kiwango cha juu, Abdul Nassib ‘Diamond Platinum’ kwa kazi zao nzuri zinazofanya vizuri nje ya Tanzania.

Rapa huyo aliweka wazi mapenzi yake kwa wasanii hao akiwa katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania, akitembelea vituo mbalimbali vya redio na televisheni pamoja na kukutana na wadau wa muziki nchini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Akiwa katika mahojiano na vituo mbalimbali vya redio, K.O alisikika akiwanadi wasanii hao huku akieleza tamaa yake ya kufanya kazi na prodyuza Nahreel, ambaye hata hivyo wameshaanza utaratibu wa kurekodi wimbo wa pamoja na prodyuza huyo kwa kumshirikisha mkali wa hip hop nchini, Joh Makini.

Hata hivyo, K.O alisisitiza kwamba amepokea beat kadhaa kutoka kwa prodyuza huyo anazotaraji kuzifanyia kazi akiwa na msanii mwenzake nchini humo, A.K.A, ambapo anadai nyimbo hizo zitakuwa katika albamu yake ijayo. “Beat zake hazisikiki kama za Afrika Kusini au Marekani, bali zinasikika vizuri na special ambazo hazipatikani kokote
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment