Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lilian alisema kuwa mara nyingi unaposhiriki unakuwa na matumaini ya kushinda na baada ya hapo uweze kufanya vitu vingi kwa jamii yako kama inavyotakiwa kwani hata waliopita walifanya hivyo, lakini inapokuja kinyume huwezi kuwa sawa.
“Nilipopata taji la urembo kutoka kwa Sitti, nilikuwa na malengo mengi sana kwa jamii yangu kama walivyofanya warembo wengine, lakini nilishindwa kwa sababu ya kufungiwa kwa mashindano hayo kwani hata kama ningeamua kufanya jambo fulani nisingeweza kwa kuwa ningetamka natokea Miss Tanzania nisingepewa msaada,” alisema Lilian.
0 comments:
Post a Comment