Mtayarishaji wa muziki na mtunzi, Lollipop amesema anatarajia kuachia albam mpya itwayo ‘Ipo Siku’.
Lollipop ambaye ameandika wimbo wa ‘Basi Nenda’ ya Mo Music pamoja na ‘Nivumilie’ ya Barakah Da Prince, ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kutoa albam hiyo ili kuwapa mashabiki wake muziki wa kutosha.
“Nimefanya muziki wa bongofleva kwa muda mrefu sana, lakini umefika wakati ya kufanya muziki ambao utawapa wanadamu chakula cha ubongo, ingawa bado nipo kama producer wa muziki na muandishi, binafsi ninanyimbo zangu nimefanya wa kwanza unaitwa Waambiane, tayari umetoka na kuna wimbo mwingine nimeachia unaitwa Ipo Siku, na sasa hivi najiandaa kufanya albam, kwaiyo albam itatoka na naamini itawafikia walengwa wote, lakini pia ni albam moja kali sana, kile ambacho nimefanya nikisikiliza binafsi naelewa nini nimefanya, albam itaitwa Ipo Siku,” alisema Pollipop
0 comments:
Post a Comment