Ikiwa inaendelea kuwajali wateja wake na kutambua umuhimu wa kuwapa kilicho bora zaidi, TECNO inakuletea simu mpya aina ya TECNO CAMON C8.
TECNO C8 ni simu iliyotukuka ikiwa na programu mama ya Android 5.0 Lollipop, uwezo wa kuhifadhi vitu wa GB 16, kioo cha HD chenye inch 5.5, lakini haikuishia hapo.
TECNO C8 ina flash katika kamera zake zote mbili yaani kamera ya mbele na kamera ya nyuma ikiwa na flash mbili. Licha tu ya kuwa na flash mbele na nyuma, TECNO C8 imeongezewa uwezo katika kamera zake ambazo ni 13 MP kamera ya nyuma, pamoja na 5 MP katika kamera ya mbele. Ukijumuisha sifa hizo mbili za flash na ukubwa wa kamera mtumiaji wa TECNO C8 atakuwa na uhakika wa kupata picha nzuri na bora zaidi hata akiwa kwenye mwanga hafifu.
Lakini pia kwa kuzingatia umuhimu wa kupiga picha za matukio ya ghafla TECNO C8 imekuja na kitufe maalum, ambacho kinaiwezesha kupiga picha hata pale kioo cha simu kinapokuwa kimezima, Mtumiaji wa simu hii anachotakiwa kufanya ni kukiminya tu kitufe hicho maalum ambacho kitaiamuru kamera ya simu kuwaka na kumwezesha kupiga picha bila kufungua simu yake.
Cha kushangaza zaidi ni pale unapoweza kuanzisha baadhi ya programu kwenye simu yako kwa kuchora tu herufi ya mwanzo wa programu hiyo juu ya kioo cha simu yako hata kikiwa kimezima.
TECNO C8 ndiyo pekee inayokuwezesha kuanzisha programu ya WhatApp kwa kuchora herufi ‘W’ katika kioo cha simu yako. Licha ya hivyo mtumiaji wa TECNO C8 anaweza kuianzisha kamera ya simu yake hata kama kioo kimezima kwa kuchora herufi ‘C’ juu ya kioo cha simu yake kikiwa kimezima.
Na mwisho kabisa haikuwasahau wale wapenzi wa muziki ndipo na wao wanapoweza kuanzisha programu ya kucheza mziki (Boom player) kwa kuchora tu herufi ‘M’ kwenye vioo vya simu zao.
Hakika TECNO wanajua nini kinastahili na kitakuwa msaada mkubwa kwa watumiaji wake, wamelibainisha ilo kwa kuunda simu hii ya TECNO C8 ambayo wameiongezea uwezo mara dufu wa kukaa na chaji.
TECNO C8 imewekewa betri yenye uwezo wa 3000mAh ambayo inaweza kudumu na chaji kwa muda wa siku 16 kwa matumizi ya kawaida, huku ikiwa na uwezo wa kupiga picha 75000 kwa wale wapenda picha, lakini pia unaweza kuangalia video kwa muda wa masaa sita na dakika thelathini. Nunua TECNO C8 yako leo na uondokane na kasumba ya kubebelea power bank.
0 comments:
Post a Comment