Madee adai hakumchukua Dogo Janja ili afanye muziki



Madee amesema hakumchukua Dogo Janja kuja Dar es Salaam ili kufanya muziki.





Madee ambaye jana amemzawadia gari Dogo Janja katika siku yake ya kuzaliwa, ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa, alimpenda Dogo Janja kutokana na ujanja wake pamoja na ucheshi aliokuwa akionesha.

“Wakati namchukua Dogo Janja kule Arusha sikudhani kama anaweza kuwa mwanamuziki mkubwa,” amesema Madee.

“Nilimchukua kwa sababu ya ucheshi wake halafu confidence. Halafu hakuogopa kuonyesha kwa watu kile alichonacho, hata kwenye gari nilikuwa nikisema mbona ni mjanja mjanja, nilikuwa nawaza kwenye kichwa chake kama akiongezewa kitu atakuwa mtu mwingine kabisa, sikuwa nadhania kabisa muziki wake kama unaweza kuja kumsaidia kabisa. Kwahiyo mimi nikamchukua kama Abdul Azizi, nikawa nikienda studio na yeye anakuja ndo na yeye akarekodi. Kwahiyo plan yangu kwa Dogo Janja ilikuwa aende shule, ndio maana nilikuwa nashughulikia mipango ya kwenda shule,” aliongeza Madee.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment