MTV Base kuanzisha kipindi kipya kwaajili ya wasanii wa Afrika Mashariki


Kituo cha MTV Base ni miongoni mwa vituo vya TV vya kimataifa vinavyo-promote kazi za wasanii wa Afrika kwa ujumla, licha ya kuwa wasanii wa Tanzania wanaopata nafasi ya kazi zao kuoneshwa bado ni ndogo kutokana na wengi wao kushindwa kufikia viwango wanavyovihitaji.






Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kuwa kituo cha kimataifa cha MTV Base kitazindua kipindi kipya kwaajili ya wasanii wa Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo Exclusive kwa Ghafla inaeleza kuwa kitakuwa ni kipindi cha saa moja kitakachoangalia maisha ya msanii kwa kumtambulisha kiundani, kuangalia jinsi alivyoweza kupata mafanikio yake pamoja na aina ya muziki anayofanya.

Hii ni habari njema zaidi kwa wasanii wa Afrika Mashariki ambao ndio walengwa wa kipindi hicho.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment