Nahreel ameiambia Bongo5 kuwa mwaka huu ni mwaka ambao amekuwa busy na kazi nyingi kuliko wakati uliopita.
“Demand ya mimi kuproduce wasanii imekuwa kubwa sana, tena sana, kupita hata maelezo,” amesema.
“Nimekuwa nikifanya kazi kwa muda mrefu zaidi hata ya kipindi cha nyuma. Mwaka huu umekuwa ni mwaka wa mafanikio kwangu na umeniweka katika nafasi nzuri sana. Kazi zangu nyingi nilizotayarisha zimefanya vizuri katika tuzo mbalimbali za kimataifa. Ngoma zinachezwa katika vituo vikubwa, hii ni kutokana na juhudi ninayoiweka katika kazi zangu,” aliongeza Nahreel.
0 comments:
Post a Comment