‘Nchi ya Ahadi’ inabaniwa kwenye baadhi ya redio – Kala Jeremiah


Rapper Kala Jeremiah amesema ingawa wimbo wake mpya ‘Nchi ya Ahadi’ unafanya vizuri lakini anashindwa kujua kwanini baadhi ya redio na TV vinashindwa kuucheza.


Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Kala alisema kutopigwa kwa wimbo huo anakuchukulia kama changamoto katika kazi yake.

“Nchi ya Ahadi ni wimbo ambao ulivyotoka na ukaingia moja kwa moja mtaani. Kwahiyo wimbo ukishaingia mtaani hauna wasiwasi, hauhitaji kuwaza, hauiutaji kusononeka, hautakiwi kufikiri nani anaupiga kwenye redio,” amesema.

Redio nyingi zimesupport lakini zipo ambazo kwa sababu moja ama nyingine ambazo mimi sijajua sababu zao za msingi. Lakini nadhani nilivyotoa video ndio ngoma ikafanya vizuri zaidi kwa sababu watu wanapenda sana. Kwa ujumla vikwazo huwa haviepukiki na huwa havikosekani katika kila kazi.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment