Hatimaye Drake amezungumza na kutoa sababu za kuamua kufanya remix hiyo, katika mahojiano aliyofanya na jarida la FADER toleo lake la 100.
Baada ya rapper huyo wa Canada kuulizwa endapo aliamua kufanya remix hiyo ili kuongeza mashabiki Afrika, alisema kuwa alijisikia tu kufanya, na hakufanya ili brand yake iwe kubwa Nigeria. Aliongeza kuwa ni heshima kubwa kwake kuwa kwenye wimbo huo.
“I just did it because I was in the moment…I wasn’t thinking like, ‘Oh man, I gotta get my brand up in Nigeria. Not to say that’s not important. I’m super-honored to be on that song….”
Drake aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza aliusikia wimbo huo wa Skepta, na ulimshawishi kufanya kitu.
Wimbo wa ‘Ojuelegba’ ambao umetokea kuwashika mastaa wengi duniani akiwemo Drake aliyeamua kufanya remix na kuzidi kumuongezea heshima Wizkid
0 comments:
Post a Comment