Nick wa Pili aanzisha taasisi iitwayo ‘Twaonekana’


Je wajua kuwa Nick wa Pili ana taasisi yake iitwayo Twaonekana? Taasisi hiyo imeanzishwa ili kuboresha ustawi wa jamii kwa kutoa elimu ya masuala mbalimbali.



Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa nafasi aliyopewa pamoja na uwezo wake anaweza kuutumia kwa ajili ya kuishawishi jamii.

“Mimi ni mwanzilishi pamoja na wenzangu watatu, Rama Kasongo na Leodgard Lazarus na wote tumegawana majukumu kutokana na experience zetu,” amesema.

“Kupitia taasisi yetu, tutakuwa tunatoa documentary za kuelimisha au zinaibua kitu fulani. Lakini mwishowe zitachangia kitu positive kwenye jamii. Tuna miradi ya kuwajengea watoto uwezo kujiendeleza wenyewe, tunafikiria kuwa na miradi ya ku-promote sanaa ili tuonekane tunatumia sanaa kuchochoa maendeleo au ustawi wa jamii,” ameongeza Nick.

“Hapa tupo kwenye hatua za kwanza lakini tumeshafanya training ya watoto Kisarawe (Kimanya Sekondari). Pia tumeshiriki matukio mbalimbali. Ndio kama tunaanza kwa sababu hatuna wadhamini tunatoa pesa mifukoni mwetu.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment